Maelezo Mafupi Kuhusu Vyuo Vya Maendeleo Ya Jamii

Maelezo Mafupi Kuhusu Vyuo Vya Vyuo Vya Maendeleo Ya Jamii Agosti 2010


1.0.        Utangulizi:

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ina vyuo tisa (9) vinavyotoa mafunzo ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Cheti cha Msingi, Cheti, Stashahada na Shahada kama ifuatavyo:-

(i)            Chuo cha Tengeru kinatoa Shahada ya kwanza kwa muda wa miaka mitatu katika Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Maendeleo na katika upangaji na uendeshaji Shirikishi wa Miradi.

(ii)          Chuo cha Missungwi kinatoa Stashahada ya Maendeleo ya Jamii Ufundi kwa muda wa miaka miwili.

(iii)         Vyuo vya Buhare, Rungemba na Monduli vinatoa Stashahada ya Maendeleo ya Jamii kwa muda wa miaka miwili

(iv)         Vyuo vya Ruaha, Uyole na Mlale hutoa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya cheti cha Msingi kwa muda wa mwaka mmoja na Cheti kwa muda wa miaka miwili.

(v)          Chuo cha Mabughai Lushoto hutoa mafunzo ya  Maendeleo ya Jamii Ufundi katika ngazi ya cheti cha Msingi kwa muda wa mwaka mmoja na cheti kwa muda wa miaka miwili.

 

Madhumuni:

-       Kutoa mafunzo ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita waliotoka moja kwa moja mashuleni.

-       Kuendeleza maafisa walioko kazini wenyewe taaluma ya Maendeleo ya Jamii au Sayansi ya Jamii;

-       Kupata wataalamu mahiri walio na uwezo wa kuiwezesha jamii kujiletea maendeleo yao wenyewe.  

-       Kuandaa mitaala inayokidhi mahitaji sanjari na mabadiliko yanayotokana na utandawazi, sayansi na teknolojia.

-       Kudurusu mitaala iliyopo ili iweze kukidhi mahitaji ya jamii kwa wakati muafaka.

 

Mahali Vyuo vilipo:

Jedwali lifuatalo linaonesha umbali wa kila chuo kutoka Makao Makuu ya Wilaya.

Jedwali Na. 1

Na.

Jina

Mkoa/Wilaya

Umbali kutoka Makao Makuu ya Wilaya

1.

Tengeru CDTI

Arusha/Arumeru

 Km  7

2.

Monduli CDTI

Arusha/Monduli

    Km  0.5

3.

Buhare CDTI

Mara/Musoma

Km 7

4.

Rungemba CDTI

Iringa/Mafinga

Km 8

5.

Missungwi CDTTI

Mwanza/Lushoto

Km 1

6.

Mabughai CDTTI

Tanga/Lushoto

   Km  16

7.

Ruaha CDTI

Iringa/Iringa

Km  5

8.

Uyole CDTI

Mbeya/Mbeya

  Km  15

9.

Mlale CDTI

Ruvuma/Songea

  Km  40

 

2.0.        HALI HALISI YA ENEO LA KILA CHUO HADI JULAI 2010

Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu sanjari na matumizi ya ardhi, maeneo mengi ya vyuo yamekuwa yakimegwa kwa kuvamiwa.  Hivyo kuna umuhimu mkubwa wa Vyuo kupatiwa hati miliki ili viweze kuendesha shughuli zake kama ilivyokusudiwa.  Jedwali Na. 2 linaonesha hali halisi ya eneo kwa kila chuo.

 

3.0.        NGAZI YA KILA CHUO KIUSAJILI

Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vinasajiliwa na Baraza la Taifa la Uthibati wa Elimu ya Ufundi (NACTE).  Vyuo huwekwa katika daraja/ngazi kutokana na kufanikiwa kwa utekelezaji wa vigezo vilivyowekwa na (NACTE).  Miongoni mwa vigezo hivyo huwa idadi na sifa za watumishi idadi na ubora wa madarasa, uwepo wa zana za kisasa za kujifunzia  na kufundishia, utayari wa uongozi wa chuo kupokea na kutekeleza maagizo ya NACTE.  Udahili wa wanachuo wenye sifa stahili na utekelezaji wa taaluma kutokana na maelekezo ya NACTE. Jedwali Na. 3 linaonesha hadhi ya kila chuo hadi kufikia Julai 2010.

Jedwali Na. 3

S/Na.

Jina la Chuo

Hadhi ya Usajili

1.

Tengeru CDTI

Full Accreditation

2.

Rungemba CDTI

Full Accreditation

3.

Missungwi CDTTI

Full Accreditation

4.

Monduli CDTI

Provisional Accreditation

5.

Buhare CDTI

Provisional Accreditation

6

Ruaha CDTI

Provisional Accreditation

7.

Uyole CDTI

Provisional Accreditation

8.

Mlale CDTI

Provisional Accreditation

9

Mabughai CDTTI

In the process of being registered

 

4.0.        UTHIBATI WA TAALUMA

Taaluma ya Maendeleo ya Jamii inatekelezwa kwa kuzingatia taratibu na kanuni zinazotolewa na kusimamiwa na (NACTE) Baraza la Taifa la Uthibati wa Elimu ya Ufundi.  Hivyo NACTE inasimamia uandaaji wa mitaala inayotumika muda wa masomo, mitihani na vigezo vyake, pamoja na ubora wa vyeti wanavyotunukiwa wahitimu kwa kila ngazi.  Jedwali Na. 4 A, B, C, na D linaonesha ngazi za mafunzo katika kila chuo na idadi ya wanachuo wa mwaka wa masomo 2009/2010.  Aidha, sehemu D ya jedwali inaonesha idadi ya wanachuo wa ngazi ya Shahada.

 

Jedwali Na. 4

A: CHETI CHA MSINGI

NTA Level

Chuo

Namba ya Wanachuo

NTA Level 4

Uyole

264

NTA Level 4

Ruaha

247

NTA Level 4

Mlale

124

NTA Level 4

Mabughai

100

 

Jumla

735

B: CHETI

NTA Level 5

Uyole

72

NTA Level 5

Ruaha

103

NTA Level 5

Mlale

88

NTA Level 5

Mabughai

60

NTA Level 5

Missungwi

38

 

Jumla

361

C: STASHAHADA

NTA Level  6

Monduli

195

NTA Level  6

Rungemba

206

NTA Level 6

Buhare

121

NTA Level 6

Missungwi

26

 

Jumla

548

D: Shahada

Mwaka

Idadi

Wa  2008/2009

122

Wa  2009/2010

137

Jumla

259

 

Key:

NTA Level 4        -           Cheti cha Msingi

NTA Level 5        -           Cheti

NTA Level 6        -           Stashahada

NTA Level 7-8     -           Shahada

 

5.0.        MAHITAJI YA WAKUFUNZI

Ili taaluma ya Maendeleo ya Jamii iweze kutekelezeka vizuri (NACTE) wametoa Idadi ya  Wakufunzi wanaotakiwa kuwepo katika Chuo.  Idadi hii ya Wakufunzi ni moja ya vigezo vya NACTE kukitambua chuo.  Jedwali Na. 5 linaonesha mahitaji ya Wakufunzi, waliopo na pungufu kwa kila chuo hadi Julai 2010.

Jedwali Na. 5

S/N

CHUO

MAHITAJI

WALIOPO

PUNGUFU

IDADI

KE

ME

1

Tengeru

50

26

16

10

24

2

Rungemba

12

10

6

4

2

3

Buhare

12

9

6

3

3

4

Monduli

12

7

5

2

5

5

Missungwi

12

11

8

3

1

6

Ruaha

12

11

7

4

1

7

Uyole

12

8

6

2

4

8

Mlale

12

7

3

4

5

9

Mabughai

12

9

7

2

3

 

JUMLA

146

98

64

34

48

 

6.0.        MAFANIKIO KATIKA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII

1.    Kupanda hadhi kwa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kutoka utoaji wa Stashada ya Juu katika Maendeleo ya Jamii na kuanza kutoa Shahada (2008/2009) katika Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Maendeleo na ile ya upangaji na uendeshaji Shirikishi wa miradi;

2.    Kuanzisha kozi za Stashahada katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vya Rungemba, Missungwi, Monduli na Buhare katika mwaka wa masomo  2008/2009.

3.    Kuanzisha kozi ya Cheti katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ruaha, Mlale na Uyole (2007/2008).

4.    Kuwezesha Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kusajiliwa na Baraza la Taifa la uthabiti wa Elimu ya Ufundi (NACTE) na kutambuliwa;

5.    Kutoa mafunzo ya Shahada, Stashahada na Cheti katika Maendeleo ya Jamii (Jedwali Na. 6, 7 na 8);

6.    Kufanya ukarabati mkubwa na mdogo katika vyuo vya Maendeleo ya Jamii pamoja na kujenga majengo mapya kama vile madarasa, mabweni na vyoo ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi.

7.    Kudurusu sera na taratibu za mitihani katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii;

8.    Kuboresha mitaala ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ili kuwa katika mfumo wa ‘Semester’ na modula kama ilvyoelekezwa na NACTE;

9.    Kununua vifaa mbalimbali vya kufundishhia na vya kujifunzia;

 

10.Kuandaa mwongozo wa wakufunzi wa kufundishia mitaala yote;

11.Kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii;

12.Kununua samani za vyuo kama vile vitanda, magodoro, viti na madawati kwa vyuo vyote tisa;

13.Kuongeza idadi ya watumishi wakufunzi na wasio wakufnzi, wenye sifa katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vyote.

14.Kuongeza idadi ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kutoka vine vya Tengeru, Missungwi, Rungemba na Buhare mwaka 2005/2006 hadi kufikia vyuo tisa mwaka 2009/20010.  Vimeongezeka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vya Monduli, Mabughai, Ruaha, Uyole na Mlale.

 

Jedwali Na. 6: Idadi ya Wanachuo Waliojiunga na Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru Ngazi ya Stashahada Ya Juu na Shahada Mwaka 2005/2006 – 2009/2010

Jedwali Na. 6

Na.

Mwaka

Wanawake

Wanaume

Jumla

 

 

Stashahada ya Juu

 

1

2005/2006

362

330

692

2

2006/2007

136

77

213

3

2007/2008

200

72

272

Jumla ndogo

1,177

4

2008/2009

48

74

122

5

2009/2010

72

65

137

Jumla ndogo

259

Jumla Kuu

188

618

1,436

           

 

 

Jedwali Na. 7: Idadi ya Wanachuo waliojiunga na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Stashahada mwaka 2005/2006 – 2009/2010

Jedwali Na.7

NA

CHUO

JINSI

2005/2006

2006/2007

2007/2008

2008/2009

2009/2010

JUMLA

1

Buhare

KE

-

-

-

50

62

112

 

 

ME

-

-

-

62

62

124

2

Rungemba

KE

-

-

-

107

144

251

 

 

ME

-

-

-

6

-

6

3

Monduli

KE

-

-

-

36

62

98

 

 

ME

-

-

-

29

47

76

4

Missungwi

KE

-

-

-

41

11

52

 

 

ME

-

-

-

9

37

46

 

JUMLA

 

 

 

 

452

455

765

NB: Vyuo hivi vilianza kutoa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Stashahada mwaka 2008/2009

Jedwali Na. 8:    Idadi ya wanachuo waliojiunga na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Cheti mwaka 2005/2006 – 2009/2010

NA

CHUO

JINSI

2005/2006

2006/2007

2007/2008

2008/2009

2009/2010

JUMLA

1

Buhare

KE

46

108

108

-

-

262

 

 

ME

50

59

34

-

-

143

2

Rungemba

KE

62

159

115

-

-

336

 

 

ME

-

-

-

-

-

-

3

Missungwi

KE

43

55

72

-

-

170

 

 

 

47

42

51

-

-

140

4

Ruaha

KE

-

-

-

86

208

294

 

 

ME

-

-

-

20

57

77

5

Uyole

KE

-

-

-

43

199

242

 

 

ME

-

-

-

30

81

111

6

Mlale

KE

-

-

-

70

96

166

 

 

ME

-

-

-

22

32

54

7

Mabughai

KE

-

-

-

35

71

106

 

 

ME

-

-

-

38

31

69

 

JUMLA

 

248

423

380

344

775

2,170

NB: Vyuo vya Buhare, Rungemba na Missungwi viliacha kutoa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya cheti mwaka 2007/2008 ambapo vyuo vya Ruaha, Uyole, Mlale na Mabughai vilianza kutoa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Cheti mwaka 2008/2009.