Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi - VMW (FCD’s)


Historia fupi ya Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi

Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (VMW) ni “Taasisi za Kiserikali” ambazo zilianzishwa mwaka 1975 kutokana na wazo la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere, baada ya kutembelea nchi ya Sweden na kuona mfumo wa elimu isiyokuwa rasmi ulivyokuwa unaendeshwa na taasisi zinazojulikana kama Folk High Schools.

Vyuo ya Maendeleo ya Wananchi vilianzishwa kama sehemu ya awamu ya tatu ya Elimu ya Watu Wazima.  Hatua ya kwanza ilihusu kuondoa ujinga wa kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu.  Hatua ya pili ilikuwa ya kuhakikisha kuwa mafanikio yaliyopatikana katika hatua ya kwanza yanakuwa endelevu na watu hawaurudii ujinga. Hatua ya tatu ilikuwa kuanzisha taasisi ambazo zingetoa maarifa na stadi kwa wananchi.  Aidha, uamuzi wa kuanzishwa VMW ulitokana na Waraka wa Baraza la Mawaziri No. 96 wa mwaka 1974 ambapo vyuo 25 vilianzishwa mwaka 1975 na kuendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kulingana na jinsi Wilaya mbalimbali zilivyo tambua umuhimu wa kuanzisha vyuo hivi. Hadi kufikia mwaka 1978, vyuo 53 vilikuwa vimeanzishwa.

Uanzishwaji wa VMW ulizingatiwa katika Sheria ya Elimu No. 25 ya mwaka 1978 chini ya Wizara ya Elimu. Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vilipoanzishwa vilirithi majengo yaliyokuwa yakitumika kwa madhumuni tofauti tofauti vikiwemo Vituo vya Mafunzo ya Maendeleo Vijijini (Rural Training Centres) ambavyo vilianzishwa mwaka 1962, Vituo vya Mafunzo ya Wakulima (Farmers Training Centres) ambavyo vilianzishwa mwaka 1963, Shule za Kati (Middle Schools) ambazo zilianzishwa mwaka 1960 na Vituo vya Mafunzo ya Ushirika vilivyoanzishwa mwaka 1964. Vyuo pekee vilivyojengwa mahsusi kuitikia wazo la Baba wa Taifa la mwaka 1975 ni vinne, vyuo hivyo ni Sengerema, Ngara, Handeni na Bigwa, ambavyo vilijengwa mwaka 1975.

 

Lengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa vyuo vya maendeleo ya wananchi (VMW)

Lengo Kuu

Lengo kuu la kuanzisha Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi lilikuwa ni kuimarisha maarifa na stadi kwa wananchi ili waondokane na ujinga, umaskini na maradhi na hatimaye kuleta maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni. 

Madhumuni mahsusi yakuanzisha VMW

Madhumuni mahsusi ya vyuo hivi yameelezwa katikaWaraka wa Serikali Na. 96 wa mwaka 1974 ambapo kipengele cha 5 kinaainisha madhumuni yafuatayo:

a)    Kumtayarisha Mtanzania ambaye ni mtu mzima aweze kukuza utu wake na kumfanya awe kamili katika jumuiya ya Watu wake;

b)   Kumtayarisha Mtanzania aweze kutumia akili zake vizuri na kuweza kuamua mambo  yake au ya Umma kwa njia iliyo sahihi;

c)    Kumsaidia Mtanzania aelewe siasa ya nchi yake na kumwezesha kushiriki kikamilifu bila woga au unafiki katika shughuli za siasa ya nchi yake;

d)    Kujenga moyo wa Mtanzania wa kushirikiana na wenzake katika shughuli au kazi za  nchi yake, na kuelewa umuhimu wa kuwa na uhusiano mwema na wenzake;

e)    Kumwezesha Mtanzania aweze kufikia kiwango cha juu zaidi katika ufundi wa kazi anazozifanya;

f)     Kumsaidia Mtanzania kukuza utamaduni wa Kitanzania; na

g)    Kuwafanya Watanzania wawe raia wenye manufaa katika Tanzania na dunia nzima.

 

Lengo na madhumuni haya yaliendelea kutekelezwa hadi mwaka 1987 ilipoundwa Tume ya Nsekela iliyoazinsha majukumu ya Wizara na Idara mbalimbali za Serikali. Tume ya Nsekela ya Februari 1987 ilibaini kuwa madhumuni na majukumu ya Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi yanashabihiana sana na yale ya Maendeleo ya Jamii ya kuwajengea uwezo wananchi ili wamudu majukumu yao vyema na kuboresha utendaji na maisha yao. Tume hiyo iliishauri Serikali kuhamishia VMW katika Idara ya Maendeleo ya Jamii.  Mwaka 1990, Serikali ilivihamishia VMW katika Idara ya Maendeleo ya Jamii chini ya iliyokuwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto. Ingawa lengo kuu halikubadilika, madhumuni yaliboreshwa ili kukidhi mabadiliko ya wakati huo katika jamii kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025.

 

Madhumuni mahsusi yaliyoboreshwa

Madhumuni yaliyoboreshwa ni yafuatayo:

a)    Kuwapatia wananchi stadi mbalimbali za ujuzi na maarifa ambayo yatawasaidia kujiajiri na kuajiriwa hivyo kuondoa umaskini katika jamii;

 

b)   Kuwawezesha viongozi katika ngazi za Vijiji na Kata kuelewa majukumu yao na hivyo kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa sera mbalimbali za Serikali za kuondoa umaskini, kuwaletea wananchi maisha bora na kusimamia misingi ya utawala bora;

 

c)    Kuwezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika maamuzi, kutambua masuala ya jinsia, kuimarisha na kudumisha utamaduni wa kupiga vita mila na desturi zinazomkandamiza mwanamke katika jamii;

 

d)    Kuziwezesha jamii kuelewa umuhimu wa hifadhi, matumizi bora ya mazingira na kutumia rasilimali zilizopo kwa faida yao; na

 

e)    Kuziwezesha jamii kuelewa na kujikinga na janga la UKIMWI.

 

Majukumu ya Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi

Ili kufikia madhumuni tajwa hapo juu VMW vimepewa majukumu mbalimbali kupitia “Mwongozo wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi” wa mwaka 2002. Majukumu hayo ni pamoja na:

a)    Kutoa mafunzo yenye kuongeza maarifa, stadi na mbinu mbalimbali za kutatua matatizo halisi ya wananchi, ili wajiletee maendeleo kwa kutumia rasilimali zilizopo;

 

b)   Kutoa mafunzo yanayokidhi mahitaji halisi ya wananchi na soko;

 

c)    Kubuni na kuendesha miradi ya uzalishaji mali na utoaji huduma vyuoni na kuvisaidia vijiji vinavyozunguka vyuo. Aidha, miradi hii ifanyiwe uchambuzi na upembuzi yakinifu ili miradi inayotekelezwa iwe na taathira chanya kwa jamii;

 

d)    Kushirikiana na asasi na mashirika mbalimbali yanayotoa mafunzo, utaalam na rasilimali nyinginezo kuwaendeleza wananchi.  Katika zoezi hili, vyuo vitapata fursa ya kubadilishana uzoefu na asasi hizo;

 

e)    Kufanya utafiti wa mahitaji utakaotoa takwimu na taarifa sahihi zitakazotumiwa na vyuo, vijiji na mitaa, katika kubuni, kupanga na kutoa mafunzo ya ushirikishwaji, pamoja na kutekeleza miradi mbali mbali ya kujitegemea.  Aidha taarifa na takwimu hizo zinaweza kutumiwa na Halmashauri za wilaya, Miji, Manispaa na Jiji katika kuandaa mipango ya uwiano ya maendeleo;

 

f)     Kuwa vituo vya kufundishia, kutengeneza na kusambaza teknolojia na nyenzo za kurahisisha kazi wafanyazo wananchi;

 

g)    Kubaini mila zisizo za maendeleo na vikwazo vingine vya maendeleo katika maeneo vilipo vyuo na kutoa mafunzo dhidi ya vikwazo na mila hizo;

 

h)    Kubuni, kuandaa na kuendesha programu mbalimbali zitakazoinua kiwango cha fikra, maarifa na stadi  za wananchi kuhusu mazingira yao na ulimwengu kwa jumla;

 

i)     Kuendesha programu mbalimbali za hifadhi ya mazingira kwa wananchi zinazohusu matumizi bora ya ardhi kwa kuzingatia kanuni za kilimo na ufugaji bora, upandaji miti na maua na utunzaji wa vyanzo vya maji;

 

j)     Kuwashirikisha wananchi katika mijadala inayohusu masuala ya jinsia;

 

k)    Kubuni mikakati ya namna ya kuwafuatilia wahitimu kwa nia ya kupima kiwango cha taathira kilichofikiwa kutokana na mafunzo yanayotolewa vyuoni, matokeo ya upimaji huo yatatumika katika kurekebisha mitaala na mikakati ya utekelezaji; na

 

l)     Kushirikiana na asasi nyingine za Serikali, madhehebu ya dini mbalimbali na Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Wananchi kubuni na kutekeleza programu na miradi madhubuti ya kutokomeza janga la UKIMWI na umaskini na kupiga vita rushwa.

 

Maeneo ya Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi

Maeneo ya vyuo vya Maendeleo ya Jamii  yamejumuisha mikoa yote 21 ya Tanzania Bara. Jedwali Na. 14 linaonesha Mikoa na Wilaya husika na idadi ya Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na baadhi ya Vyuo vya Ufundi Stadi vilivyotembelewa.

Jedwali Na 1: Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi

Na

Mkoa

Wilaya

Chuo

Idadi yaWilaya

Idadi ya Vyuo

1

Arusha

Monduli

Monduli FDC

1

1

2

Dar es Salaam

Ilala

Arnautoglu FDC

2

2

Temeke

Chang’ombe

3

Dodoma

Mpwapwa

Chisalu FDC

2

2

Kondoa

Munguri FDC

4

Kagera

Biharamulo

Rubondo FDC

4

4

Bukoba (M)

Bukoba RVT&SC

Bukoba (V)

Gera FDC

Ngara

Ngara FDC

5

Kilimanjaro

Moshi (V)

Msinga FDC

4

4

Moshi (M)

Moshi RVT&SC

Rombo

Mamtukuna FDC

Same

Same FDC

6

Kigoma

Kasulu

Kasulu FDC

3

3

Kibondo

Kibondo FDC

Kigoma

Kihinga FDC

7

Iringa

Kilolo

Ilula FDC

2

3

Njombe

Njombe FDC

Njombe

Ulembwe FDC

8

Lindi

Lindi (V)

Chilala FDC

2

2

Kilwa

Kilwa Masoko FDC

9

Manyara

Mbulu

Tango FDC

1

1

10

Mara

Musoma

Musoma FDC

3

3

Tarime

Tarime FDC

Bunda

Kisangwa FDC

11

Mtwara

 

 

Masasi

 

 

Masasi FDC

 

 

3

 

 

4

Masasi VTC

Mtwara

Mtawanya FDC

Newala

Newala FDC

12

Morogoro

Morogoro

Bigwa FDC

4

5

Kilosa

Kilosa FDC

Mikumi VTC

Ifakara

Ifakara FDC

Ulanga

Sofi FDC

13

Mwanza

Maswa

Malya FDC

5

5

Misungwi

Misungwi CDTI

Mwanza (M)

Mwanza RVT&SC

Mwanza (V)

Karumo FDC

Sengerema

Sengerema FDC

14

Mbeya

Rungwe

Katumba FDC

2

2

Mbeya (M)

Nzovwe FDC

15

Pwani

Kibaha

Kibaha FDC

3

3

Kisarawe

Kisarawe FDC

Ikwiriri

Ikwiriri FDC

16

Tabora

Sikonge

Sikonge FDC

3

4

Urambo

Urambo FDC

Nzega

Nzega FDC

Nzega

Mwanhala FDC

17

Tanga

Handeni

Handeni FDC

3

3

Muheza

Kiwanda FDC

Lushoto

Mabughai CDTI

18

Rukwa

Mpanda

Msaginya FDC

2

2

Nkasi

Challa FDC

 

19

 

Ruvuma

 

Mbinga

 

Mbinga FDC

 

3

 

3

Songea (V)

Muhukuru FDC

Tunduru

Nandembo FDC

20

Singida

Singida

Singida FDC

2

2

Iramba

Msingi  FDC

21

Shinyanga

Shinyanga (M)

Buhangija FDC

4

4

Geita

Mwanva FDC

Maswa

Malampaka FDC

Bariadi

Bariadi FDC

Jumla

56

62

 

Stadi zinazotolewa katika VMW

Katika VMW ilibainika kuwa stadi zinazotolewa ni pamoja na hizi zifuatazo:

a)    Upishi;

b)   Kilimo na Ufugaji;

c)    Ufundi umeme wa majumbani;

d)    Ufugaji samaki na nyuki;

e)    Ususi na ufumaji;

f)     Usindikaji wa vyakula na matunda;

g)    Ushonaji;

h)    Uchomeleaji vyuma;

i)     Umekanika;

j)     Kompyuta;

k)    Useremala;

l)     Uashi;

m)  Utengenezaji mapambo;

n)    Ujasiriamali;

o)   Uendeshaji hoteli; na

p)   Umeme  wa magari

Kikosi kazi kilithibitisha kuwa VMW vinatoa mafunzo kulingana na mazingira husika hivyo stadi zinatofautiana kutoka chuo kimoja hadi kingine.

 

Jedwali Na. 18: Mafunzo/Stadi katika kila Chuo

Na

Mikoa

Wilaya

Chuo

Stadi Zilizopo

Stadi za Ziada

1

Arusha

Monduli

Monduli FDC

Useremala, Uashi, Ushoni, Udereva, Kompyuta, Kilimo,  Ufugaji, Upishi na Lishe na Ufundi Chuma

Ufundi Chuma, Ufundi Magari, Udereva, Ujasiriamali, Ushonaji, Useremala, Uashi, Umeme, Uungaji Vyuma, Ufundi Bomba, Umeme wa Magari, Kilimo na Ususi.

2

Dar es Salaam

Ilala

ArnautogluFDC

Biashara, Umeme na Ufundi wa Magari

Ufundi Viatu, Kompyuta, Udereva, Ufundi Magari, Ufundi Bomba, Uchomeleaji na Ufundi Rangi

3

Dodoma

Mpwapwa

Chisalu FDC

Useremala, Maarifa ya Nyumbani  na  Kilimo 

Kompyuta, Udereva, Ufugaji,Ufundi Magari, Secretatarial, Ufundi Bomba, Uchomeleaji na Ufundi Rangi

Kondoa

Munguri FDC

Useremala, Uashi,ushonaji, Upishi na lishe

Ufundi Magari, uchomeleaji, Umeme wa Majumbani, Umeme Jua, Udereva, Kompyuta, Uhazili, Ufundi Bomba, Uchomeleaji na Ufundi rangi

4

Kagera

Biharamulo

Rbondo FDC

Ushonaji (Sayansi Kimu), Uashi, Useremala na Ufundi Chuma.

Kilimo, Ufugaji, Ujasiliamali, Kompyuta, Electronics, Umeme wa Majumbani, Uungaji Vyuma, MV Mechanics, Udereva, Ujenzi Barabara, Kompyuta na Upishi.

Bukoba (M)

Bukoba RVT&SC

-

-

 

Bukoba (V)

GeraFDC

S/Kimu, Useremala, Uashi, Mafunzo ya muda mfupi – UKIMWI, Kilimo na Uchaguzi.

Umeme  wa Majumbani, Uchomeleaji, Kompyuta, Electronics, Usindikaji, Umeme wa Magari, Mv Mechanics, Udereva, Kupiga Chapa, Kilimo na Catering.

Ngara

Ngara FEDC

Ushonaji, Uashi, Useremala, Ufundi magari, Udereva, Bidhaa za ngozi, mafunzo ya Uelewa

Ushonaji, Uashi, Uchomeleaji vyuma, Umeme wa Magari, Umeme wa Majumbani, Electonics, Usindikaji Mazao, Ushonaji Bidhaa za Ngozi, Useremala, Kompyuta, Ufundi Bomba, Upishi, Ufundi Rangi, Kilimo na Ufugaji.

5

Kilimanjaro

Moshi (V)

Msinga FDC

Useremala, Uashi,ufundi magari, Ushonaji, Upishi na Lishe, Umeme wa Majumbani, Udereva, Ufundi Bomba,  Kompyuta, Kilimo na Ufugaji

Umeme, Ufundi Magari, Uchomeleaji, Ufundi Bomba, Ufundi Rangi, Electronics na Uchimbaji Madini, Userermala, Uashi, Umakenika, Udereva, Kilimo na Ufugaji

Rombo

Mamtukuna FDC

Useremala, Uashi, Ufundi Magari, Kilimo, Ufugaji, Upishi na Lishe, Ushonaji na Kompyuta

Ufundi Magari, Ufundi Bomba, Upambaji, Kompyuta, Ujasiriamali, Useremala, Uashi, Udereva, Uafundi wa Friji, Ufundi Umeme wa Majumbani, Upishi na Lishe, Kilimo na Ufugaji

Same

Same FDC

Kompyuta, Udereva, Ufundi Magari, Kilimo, Ufugaji, Useremala, Ushonaji.

Umeme, Ufundi Magari, Ufundi Bomba, Upambaji, Kompyuta, Ujasiriamali, Useremala, Uchomeleaji, Udereva, Umakenika wa Kilimo, Electronics, Ufundi Friji na Usanii

6

Kigoma

Kasulu

Kasulu FDC

Kilimo, Ufugaji, Usremala, Uashi, Ushonaji (S/Kimu), Umakenika.

Computer Maintenance, ICT, Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Kilimo cha Mitambo na Matengezo yake, Ushonaji, Uashi, Kilimo cha Matunda, Ufundi Bomba, Ufundi Magari, Uashi, Useremala, Uungaji Vyuma, Upishi na Uhazili.

Kibondo

Kibondo FDC

Uashi, Umakanika, Upishi, Kilimo na Ushonaji.

Useremala, Uashi, Umakenika, Kilimo, Kompyuta, Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Utengenezaji wa Majokofu, Utengezaji wa Barabara, Uhazili, Ufundi Magari, Uungaji  Vyuma, Ufundi Bomba, Ufundi Rangi na Uchoraji, Udereva na Ufundi Viatu.

Kigoma

Kihinga FDC

Ushonaji, Uashi, Umakanika, Upishi, na Kilimo.

Useremala, Uashi, Umakenika, Kilimo, Kompyuta, Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Utengenezaji wa Majikofu, Utengezaji wa Bara bara, Mafunzo ya Uelewa, Ufundi Magari, Uungaji Vyuma, Umeme, Kompyuta, Lishe na Upishi, Ufundi Bomba na Udereva.

7

Iringa

Kilolo

Ilula FDC

Useremala, Uashi, Ushonaji, Ufumaji, Kilimo cha mboga, Ufugaji wa ng’ombe na Computer

Ufundi magari, Mafunzo ya Computer, Udereva, Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Udereva, Kilimo, Ufugaji, Ufundi Bomba na Uungaji Vyuma.

Njombe

Njombe FDC

Useremala, Uashi, Umeme, Ufundi magari Ushonaji,

Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Uchomeleaji, Ufundi Bomba, Udereva, Upishi, Hotel Management, Userermala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Udereva, Kilimo, Ufugaji, Uungaji Vyuma na Kompyuta.

Njombe

Ulembwe FDC

Useremala, Uashi, Ushonaji, Umeme majumbani.

Umeme wa Majumbani, Ufundi wa Magari, Uungaji Vyuma, Udereva, Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Kilimo, Ufugaji, Ufundi Bomba, Kompyuta na stadi zilizopo sasa ziendelee,

8

Lindi

Lindi (V)

Chilala FDC

Useremala, Ufumaji, Kilimo, Mifugo, Mafunzo nje ya Chuo na Mafunzo ya Muda Mfupi.

Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Uchomeleaji, Ufundi Bomba, Udereva, Upishi, Hotel Management, Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Kilimo, Ufugaji na Kompyuta.

Kilwa

Kilwa Masoko FDC

Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Ufumaji, Kilimo, Mifugo, Mafunzo nje ya Chuo na Mafunzo ya Muda Mfupi.

Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Kompyuta, Uchomeleaji, Ufundi Bomba, Udereva, Upishi, Hotel Management, Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Kilimo, Ufugaji, Uungaji Vyuma na Ujasiriamali,

9

Manyara

Mbulu

Tango FDC

Useremala na Ushonaji

Userermala, Uashi, Umakenika, Kilimo, Ufugaji, Umeme, Ufundi Umeme mbadala, Ufundi Magari, Udereva na Ujasiriamali

10

Mara

Musoma

Musoma FDC

Uashi, Kilimo, Upishi, Ushoni na Useremala

Kilimo; Udereva; Uvuvi; Utengenezaji wa Maboti/Mashua; Useremara; Uashi/Ujenzi; Ushonaji; Umeme; Ufundi Magari, Upishi, Uendeshaji Canteen, Hotel Management, Umeme wa Magari, Udereva na Kompyuta

Tarime

Tarime FDC

Ushonaji, Useremala, Umeme na Uashi.

Computer, Udereva, Kilimo, Mechanics, Ujasiliamali, Useremala, Umeme, Udereva, Kompyuta na Uchomeaji Vyuma.

Bunda

Kisangwa FDC

Useremala, Ushonaji, Upishi na Uashi.

Umeme, Mechanics, Udereva, Ufundi Bomba, Kilimo, Useremala, Welding, Ufugaji, MV Mechanics na Hotel Management.

11

Mtwara

Masasi

Masasi FDC

Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Umeme wa majumbani, Upishi na Elimu ya Sekondari.

Usindikaji, Ujasiliamali, Udereva, Uchomeleaji, Hotel Management. Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Kilimo, Ufugaji, Ufundi Bomba, Uungaji Vyuma na Kompyuta.

Mtwara

Mtawanya FDC

Useremala, Ujenzi, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Kilimo, Uraia na Udereva

Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Uchomeleaji, Udereva, Upishi, Hotel Management, Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Udereva, Kilimo, Ufugaji, Ufundi Bomba na Kompyuta.

Newala

Newala FDC

Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Ufumaji, Magari, Kilimo, Umeme wa majumbani, Uchomeleaji

Udereva, Kompuyta, ICT, Hotelia, Userermala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Kilimo, Ufugaji, Ufundi Bomba, Uungaji Vyuma,  Electronics na stadi zote zilizopo sasa ziendelee.

12

Morogoro

Morogoro

Bigwa FDC

Useremala, Uashi, Ushonaji, Upishi na Lishe, Umeme wa Majumbani, Ufundi Magari na Elimu ya Chekechea.

Uchomeleaji, Ujasiliamali, Usindikaji wa Vyakula, Udereva, Upishi, Upambaji, Uhifadhi wa Vyakula, Ufundi Magari, Uashi, Kompyuta, Kilimo na Ufugaji

Kilosa

Kilosa FDC

Useremala, Ushonaji,  Kilimo na Ususi

Kilimo cha Matunda, Uashi, Uchomeleaji, Electronics, Umakenika, Udereva, Kilimo, Ufugaji na Umeme.

Ifakara

Ifakara FDC

Useremala, Uashi, Ushonaji, Kilimo, Mifugo na Sanyansi Kimu

Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Kompyuta, Uchomeleaji, Ufundi Bomba, Udereva, Upishi, Hotel Management, Useremala, Uashi, Kilimo, Umeme na stadi za sasa na elimu ya sekondari ziendelee.

Ulanga

Sofi FDC

Uashi, Useremala, Ushonaji, Kilimo, Ufugaji, Sayansi Kimu na Upishi.

Useremala, Ushonaji, S/Kimu, Kilimo, Ushonaji, Umeme, Uungaji Vyuma, Ufundi Bomba, Umeme wa Magri, Ususi na Ujasiriamali.

13

Mwanza

Maswa

Malya FDC

Kilimo, Ufugaji, Useremala, Ushonaji, Uashi na Welding.

Mechanics, Computer, Udereva, Upishi, Umeme, Uungaji Vyuma, Kilimo, Ufugaji, Kompyuta na Catering.

Misungwi

Misungwi CDTI

-

-

 

Mwanza (M)

Mwanza RVT&SC

-

-

Mwanza (V)

Karumo FDC

Kilimo, Useremala, Ushonaji na Uashi

Umeme, Udereva, Uvuvi, Ushonaji, Uashi, Useremala, Uungaji Vyuma, Umeme, Ufundi Magari, Utengenezaji bidhaa za Ngozi na stadi za sasa ziendelee.

Sengerema

Sengerema FDC

Welding, Hifadhi za Mazao, Mazingira, UKIMWI, Kilimo na Udereva.

Ujasiliamali, Usindikaji mazao ya Kilimo, Kompyuta, Uashi, Uvuvi, Umeme, Kuunga Vyuma, Uashi, Useremala, Ushonaji, Udereva, Makenika, Mama Lishe, Kilimo na Ufugaji.

14

Mbeya

Rungwe

Katumba FDC

Useremala, Umeme, Uashi, Ushonaji, Hotel Management, Biashara, UKIMWI, Kilimo

Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Kompyuta, Uchomeleaji, Ufundi Bomba, Udereva, Upishi, Hotel Management, Uashi, Umakenika, Kilimo, Ufugaji, Electronics na stadi za sasa ziendelee.

Mbeya (M)

Nzovwe FDC

Uashi, Useremala, Ushonaji na Kilimo.

Kompyuta,Elctronics,Umakenika, Umeme wa Magari, Umeme wa Majumbani, Udereva, Upishi na Hotel Managaement, Uashi, Uungaji Vyuma, Ufundi Bomba, Kilimo, Ususi, S/Kimu na Ujasiriamali

15

Pwani

Kibaha

Kibaha FDC

Useremala, Uashi, Umeme Majumbani, Ufundi Chuma, Ufundi Magari, Udereva, Upishi, Menejimenti ya Hotel, Ushonaji, Kilimo, mifugo na Ufundi Bomba

Ufundi Viatu, Ufundi Magari, Kompyuta, Secretarial,  Uchomeleaji na Ufundi Rangi na stadi za sasa ziendelee

Kisarawe

Kisarawe FDC

Kompyuta, Udereva, Ufundi Magari, Kilimo, Ufugaji, Useremala na Ushonaji

Umeme, Ufundi Bomba, Upambaji, Kompyuta, Ujasiriamali, Useremala, Udereva, Ufundi Magari, Uhazili, Uchomeleaji na Ufundi Rangi

Ikwiriri

Ikwiriri FDC

Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Ufumaji, Kilimo, Mifugo, Mafunzo nje ya Chuo na Mafunzo ya Muda Mfupi.

Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Kompyuta, Uchomeleaji, Udereva, Upishi, Hotel Management, Kilimo, Ufugaji, Ufundi Bomba, Uungaji Vyuma, Electronics na Umeme Jua na stadi za sasa ziendelee.

16

Tabora

Sikonge

Sikonge FDC

Uashi, Useremala, Ushonaji na Kilimo.

Kompyuta, Elctronics, Umakenika, Umeme wa Magari, Umeme wa Majumbani, Udereva, Upishi na Hotel Managaement, Uashi, Umeme, Uungaji Vyuma, Ufundi Bomba, Umeme wa Magri, Kilimo na Ususi.

Urambo

Urambo FDC

Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Ufumaji, Kilimo, Mifugo, Mafunzo nje ya Chuo na Mafunzo ya Muda Mfupi.

Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Uchomeleaji, Ufundi Bomba, Udereva, Upishi, Hotel Management, Udereva, Kilimo, Ufugaji, Kompyuta na stadi za sasa ziendelee.

Nzega

Nzega FDC

Useremala, Uashi, Ushoni, Udereva, Kompyuta, Ufugaji na Kilimo

Umeme, Ufundi Magari, Uchomeleaji, Ufundi Bomba, Ufundi Rangi, Electronics, Uchimbaji Madini, Uashi, Umakenika, Ufugaji na Umeme

Nzega

Mwanahala FDC

Useremala, Uashi, Ufundi Magari, Kilimo, Ufugaji, Ushonaji, Upishi na Lishe.

Uumeme, Ufundi Magari, Ufundi Bomba, Upambaji, Kompyuta, Ujasiriamali, Useremala, Uashi, Udereva, Ufundi wa Friji, Upishi na Uendeshaji wa Migahawa

17

Tanga

Handeni

Handeni FDC

Ushonaji, Useremala, Upishi na Lishe, Uashi, Menejimenti ya Hotel, Umeme wa Majumbani, Ufundi Magari na Kompyuta

Ujasiriamali, Kompyuta, Uchomeleaji, Udereva, Uhandisi wa Kilimo, Electronic, Ufundi Friji na Usanii

Muheza

Kiwanda FDC

Useremala, Uashi, Upishi na Lishe, Ushonaji na Kilimo, Ufugaji na Ujasiriamali

Udereva, Ufundi Magari, Uashi, Ufundi wa Friji, Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Upishi na Uendeshaji wa Migahawa.

Lushoto

Mabughai CDTI

-

-

18

Rukwa

Mpanda

Msaginya FDC

Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Kilimo, Mifugo, Ujasiliamali.

Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Kompyuta, Uchomeleaji, Ufundi Bomba, Udereva, Upishi, na Hotel Management, Userermala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Kilimo, Ufugaji, Electronics na zilizopo ziendelee.

Nkasi

Challa FDC

Uashi, Useremala, Ushonaji na Kilimo.

Useremala, Uashi, Ushonaji, Kilimo, Umeme na Computer, Ushonaji, Useremala, Uashi, Umeme, Uungaji Vyuma, Ufundi Bomba, Umeme wa Magri, Kilimo, Ususi S/Kimu na Ujasiriamali.

19

Ruvuma

Mbinga

Mbinga FDC

Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Ufumaji, Kilimo, Mifugo, Mafunzo nje ya Chuo na Mafunzo ya Muda Mfupi

Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Kompyuta, Uchomeleaji, Ufundi Bomba, Udereva, Upishi, Hotel Management, Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Kilimo, Ufugaji, Electronics na zilizopo sasa ziendelee.

Songea (V)

Muhukuru FDC

Uashi, Useremala, Ushonaji Kilimo, Ufundi Magari, Umeme na Mifugo

Kompyuta, Elctronics, Umakenika, Umeme wa Magari, Umeme wa Majumbani, Udereva, Upishi, Hotel Managaement, Ushonaji, Uselemala, Ufugaji, Uashi, Uungaji Vyuma, Ufundi Bomba, Kilimo, Ususi, S/Kimu na Ujasiriamali.

Tunduru

Nandembo FDC

Useremala, Uashi na Ushonaji

Kilimo, Ufugaji, Kompyuta, Uchomeleaji, Ufundi Bomba, Udereva, Upishi, Hotel Management, Useremala, Uashi, Ushonaji, Umakenika, Kilimo, Ufugaji na  stadi zilizopo ziendelee.

20

Singida

Singida

Singida FDC

Useremala,Uashi, umeme wa nyumbani,ushoni, na upishi na lishe

Ufundi Magari, Udereva, Kompyuta, Menejimenti ya  Hoteli na Utalii, Userermala, Uashi, Umakenika, Kilimo, Ufugaji na Umeme

Iramba

Msingi  FDC

Useremala, Upishi, Ushonaji, Uchomeleaji Chuma.

Kilimo, Ushirika, Ufugaji wa nyuki na Urinaji wa asali, Upishi na Lishe, Udereva, Ufundi Magari, Uashi, Udereva, Ufundi wa Friji, Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Upishi na Uendeshaji wa migahawa.

21

Shinyanga

Shinyaga (M)

Buhangija FDC

Ushonaji, Upishi, Ujasiliamali, Useremala, Umeme Majumbani, Uchomeleaji, Stadi za Maisha na Masomo ya Jioni.

Mitambo na Magari, Ufundi Bomba, Udereva, Uashi, Kompyuta, Upambaji, Usindikaji Mazao, Umeme wa Magari, Umeme, Useremala, Ushonaji, Upishi, Uungaji Vyuma, Uashi, Kilimo, Ufugaji na Hotel Management na stadi za sasa ziendelee.

Geita

Mwanva FDC

Umeme wa Majumbani, Uashi, Useremala, Umakenika, Kompyuta, Udereva, Kilimo, Ushonaji na Welding.

Ufundi Bomba, Ujasiliamali, Umeme wa Mgari, Electronics, Fitter Mechanics, IT, Ushonaji, Useremala, Uashi, Uhazili, Kompyuta, Ufundi Magari, Uungaji  Vyuma, Umeme Majumbani, Ufundi Rangi, Uchoraji, Kilimo, Udereva na Ufundi Viatu.

Malampaka

Malampaka FDC

Kilimo, Ufugaji, Useremala, Uashi, Ujasiriamali.

Udereva; Kilimo; Ufugaji; Welding; Fitter Mechanics na Mv Mechanics, Ushonaji, Useremala, Uashi, Umeme, Mv Mechanics, Udereva, Catering & Hotel Management na Computer Applications

Bariadi

Baradi FDC

Useremala, Kilimo, Uashi, Ushonaji, Udereva, Ujasiliamali, Elimu ya Biashara, Elimu ya Jinsia, Elimu ya UKIMWI na Uraia.

Kompyuta, Umakenika, Ufundi Chuma, Uchmeleaji, Umeme wa Majumbani, Umeme wa Magari, Electronics, Udereva, Ufundi Magari, Useremala, Ushonaji, Upishi, Kilimo, Uungaji Vyuma, Uchongaji Vyuma, Ufundi Bomba, Uchoraji na Ufundi Rangi.

 

Ambatisho Na. 1: Mafunzo yanayotolewa katika Vyuo vya Ufundi Stadi nchini

S/N

Training Area

Occupations

1

Building Construction

1.1 Masonary & Bricklaying

1.2 Capentry & Joimery

1.3 Plumbing & Pipe Fitting

1.4 Painting and Decoration

2

Metal Work

2.1 Welding and Fabnrication

2.2 Blacksmithing

2.3 Fitter Mechanics Work

3

General Maintenance and Mechanics

3.1 Motor Vehicle Mechanics

3.2 Agro – Mechanics

3.3 Motor Cycle/Bicycle Maintenance

4

Electrical Installation

4.1 Domestic Electrical Inatallation

4.2 Telecommunications

5

Clothing and Textile

5.1 Tailoring

5.2 Tie and Dye

5.3 Batik

5.4 Handloom Weaving

6

Agriculture and Food Processing

6.1 Crop Production

6.2 Horticulture

6.3 Floriculture

6.4 Meat Processing Technology

6.5 Mushroom Production

6.6 Dairy Production

6.7 Wine Making

6.8 Poultry Production

6.9 Vegetable Production

6.10 Vegetable Processing

6.11 Animal Husbandry

7

Hotel & Services

7.1 Food Production

7.2 Food & Beverage Services

7.3 House Keeping

7.4 Front Office