highlights


Reports and Policies

News and Events

Hotuba ya Mh. Margaret Sitta kwenye Kongamano la Wanawake Wajasiriamali Dar-es-Salaam

HOTUBA YA MH. MARGARET SITTA (MB), WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO KWENYE KONGAMANO LA WANAWAKE WAJASIRIAMALI LILILOFANYIKA TAREHE 18 AGOSTI, 2009 KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE, DAR ES SALAAM.

Mhe. Anne Kilango Malecela (Mb), Mbunge wa Same Mashariki,
Ndugu Christine Kilindu, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI),
Ndugu Moses Emmanuel, Afisa Mtendaji Mkuu was ‘East Africa Speakers Bureau’ (ESB),
Dr. Victoria Kisyombe, Afisa Mtendaji Mkuu SELFINA,
Ndugu Suzan F. Mashibe, Mkurugenzi Mtendaji, Tanzania Jet Centre,
Ndugu Subira Mchumo, Afisa Mtendaji Mkuu Studio 7,
Wageni Waalikwa,
Ndugu Wanahabari,
Mabibi na Mabwana,

Ndugu washiriki,
Awali ya vote, napenda kuwashukuru waandaaji wa kongamano hili kwa kunialika kuja kulifungua. Nimefurahi sana kupata fursa hii ya kuonana na kuzungumza nanyi wanawake wenzangu, wajasiriamali mliojiajiri na mlioajiriwa katika mkutano huu muhimu kwa maendeleo yetu. Ushiriki wenu katika mkutano huuunaonesha kuwa mnatambua na kuthamini umuhimu wa kukutana, kubadilishana mawazo na kuibua mbinu mpya za kujiendeleza katika fani zenu mbali mbali.

Ndugu Washiriki,
Nalipongeza Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na East Africa Speakers Bureau kwa kuandaa mikutano kama hii kila mwaka. Hii inaonesha kuwa taasisi hizi zinatambua umuhimu wa wanawake katika maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla. Ni vigumu kwa nchi yoyote, ikiwemo Tanzania kufanikiwa kiuchumi kama wanawake wajasiriamall hawatashiriki na kujumuishwa katika kupanga mikakati ya maendeleo. Hakuna ubishi kuwa kihistoria wanawake wametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi ingawa mara nyingi mchango wao hautambuliki wala kuth9miniwa na jamii. Kwa sababu hii, naomba muungane nami kutambua jitihada za CTI na ESB katika kuandaa mkutano huu ambao, pamoja na mambo mengine, unalenga kutambua nafasi ya wanawake katika maendeleo.

Ndugu Washiriki,
"Kongamano la Wanawake Wajasiriamali"; "walioajiriwa na waliojiajiri" na kauli mbiu yake "Uongozi, Mabadiliko na Ubunifu" ni mambo yaliyofikiriwa na kuletwa mbele yetu katika wakati muafaka. Nisingependa kuchukua muda wenu mwingi kuzungumzia umuhimu wa ujasiriamali kwa wanawake kwani sote hapa tumefika kwa kuwa tunaelewa umuhimu wa ujasiriamali kwa wanawake wenyewe, familia zao na taifa kwa ujumla.

Matokeo ya tafiti mbalimbali yanaonesha kuwa wanawake wanafanya kazi kwa muda mrefu zaidi kuliko wanaume (hufanya kazi masaa 16 - 18 kwa siku) na wamekuwa nguzo katika maendeleo ya familia na jamii kwa miaka mingi sana., Wanawake wamekuwa wakiwekwa kando katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali na maendeleo lakini kwa hivi sasa, hili linaendelea kupungua taratibu kutokana na jitihada zinazofanywa na watu na taasisi mbalimbali kubadilisha mtazamo huu. Ndiyo sababu tupo hapa lea ili tuhamasishane kutokomeza dhana hii potofu. Mkutano huu unathibitisha kwamba wanawake wanaweza kufanya chochote na kufanikiwa kama wanaume. Hakika, mtazamo uliomkandamiza mwanamke umepitwa na wakati!

Ndugu Washiriki,
Kauli mbiu ya leo; Uongozi, Mabadiliko na Ubunifu inatambua kuwa dunia inabadilika kila siku. Leo tuna soko huria, kuna mtikisiko wa uchumi duniani na mambo mengi ambayo awali hayakuwepo. Kama mwanamke mjasiriamali uliyeajiriwa au kujiajiri, inabidi ubadilike kulingana na dunia inavyokwenda. Mafanikio katika mabadiliko haya yanahitaji uongozi thabiti na kuwa na utaratibu wa kujifunza na kubadi/ishana uzoefu na wakufunzi au wenzetu waliofanikiwa zaidi. Iii tuweze kushindana vema katika sako huria, inabidi tuwe wabunifu na tutafakari huduma tunazotoa, jinsi ya kuziboresha na kuzitofautisha na nyingine huku tukibuni bidhaa bora au huduma mpya.

Ndugu Washiriki,
Ninatambua kuwa watakaozungumza lea ni wanawake wajasiriamali waliofanikiwa katika ajira ama biashara zao. Kuwepo kwao hapa lea ni fursa nzuri na ya kipekee katika maendeleo yetu. Pamoja na shughuli zao nyingi za kiuchumi, kijamii na siasa, wenzetu hawa wamekubali kuja kujumuika nasi lea ili kutueleza walivyofika hapo walipofikia.

Ndugu Washiriki,
Mwaka jana kwenye mkutano kama huu nilisema kuwa Serikali ina mpango wa kufungua Benki ya Wanawake. Nina furaha kubwa kuwajulisha kuwa benki hiyo imefunguliwa rasmi tarehe 28/7/2009 na imeanza kutoa huduma. Kufunguliwa kwa Benki ya Wanawake Tanzania kunatoa fursa ya wanawake kujenga tabia ya kuweka akiba na kujifunza kuwekeza kwa kununua hisa. Ninawaasa wanawake wote pia kuwashawishi wanaume kujiunga na Benki hii ambayo haina ubaguzi wa jinsi. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuhakikisha kuwa wanawake wanafanikiwa kwa kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyowakera wanawake siku hadi siku.

Ndugu Washiriki;
Kama mnavyofahamu, tarehe 25 Oktoba, 2009 kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini kote. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto pamoja na majukumu mengine iliyo nayo, imepewa pia jukumu la kusimamia azma ya kufikia asilimia 50 ya uwakilishi wa wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi wa kisiasa, kiutendaji na nafasi za maamuzi. Wizara inawahimiza Wanawake kujitosa katika kuwania nafasi za uongozi kutokana na ukweli kwamba wapo wanawake wengi walio na uwezo wa kuongoza kwani wanawake waliopewa fursa za kuongoza wamethibitisha kuwa wanaweza. Mwanamke ni kitovu cha maendeleo katika jamii na tutumie mtazamo huu kujiendeleza.
Baada ya kusema hayo, sasa natangaza kuwa kongamano hili limefunguliwa rasmi.
Nawashukuru sana kwa kunisikiliza na nawatakia Kongamano lenye mafanikio.