highlights


Reports and Policies

News and Events

Hotuba ya Mhe. M.J. Mwaffisi kwenye mkutano wakuandaa viashiria vya mkataba wa kuondoa ubaguzi

Hotuba ya Mhe. M.J. Mwaffisi aliyoitoa kwenye ufunguzi wa mkutano wa kikazi wa kuandaa viashiria vya mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake katika ukumbi wa Taasisi ya Elimu Tanzania, KIJITONYAMA 29/08/2008

Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufika hapa kufungua mkutano huu muhimu. Nimefurahishwa na ushiriki wenu ambao umeweza kuwakutanisha washiriki kutoka Wizara za Serikali, Maafisa wa Mkoa wa Dar es Salaam na Wilaya zake, Vyama vya Wafanyakazi na Mashirika ya Kidini. Mikutano kama hii ni hatua mojawapo inayowezesha watumishi na wafanyakazi kutoka katika maeneo mbalimbali kufahamiana na kubadilishana uzoefu.