highlights

Reports and Policies

News and Events

Mkutano kati ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto na ujumbe wake Msumbiji

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mheshimiwa Sofia Simba (Mb) tarehe 04 Machi 2011, alikutana na ujumbe wa Umoja wa Wanawake wa Msumbiji ulioongozwa na Balozi wa Msumbiji hapa nchini Mheshimiwa Amour Zacarias na Bibi Caterina Pajume ambaye ni mwakilishi katika Tume ya Hifadhi ya Chakula nchini Msumbiji.

image
Bibi Caterina Pajume mwakilishi wa wanawake wa Msumbiji (katikati) akikabidhi barua ya mwaliko wa Mkutano Mkuu wa wanawake wa Msumbiji kwa Waziri Mhe. Sofia Simba (Mb) Ofisini kwake,

Ujumbe huo umekuja na mwaliko kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kupata wajumbe wanawake watakao hudhuria Mkutao Mkuu wa Tatu wa Umoja wa Wanawake wa Msumbiji ambao utafanyika tarehe 26- 30 Aprili, 2011. Bibi Pajume pia aliwasilisha salaam maalum za Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Msumbiji kwa Mheshimiwa Sofia Simba (Mb) kwa niaba ya Wanawake wote wa Tanzania.

Ujumbe huu umeletwa hapa Tanzania tarehe 04 Machi; ambapo tarehe kama hiyo mwaka 1967 ni siku ambayo wanawake wapiganaji wa Msumbiji waliunda umoja wao katika harakati za kudai uhuru na hivyo kutoa mchango mkubwa wa ukombozi wa wananchi wa Msumiji na kudhihirisha kwamba wanawake siyo viumbe dhaifu wasiyo na machango thabiti katika jamii na taifa kwa ujumla.