MCDGC Publication

Mpango wa Taifa wa Kukabiliana na Ukatili Dhidi ya Watoto

Kikosi Kazi Kinachojumuisha Sekta Mbalimbali: Mpango wa Taifa wa Kukabiliana na Ukatili Dhidi ya Watoto

Ripoti ya Dunia ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukatili dhidi ya Watoto ambayo ilifanyika kuanzia mwaka 2001 na kukamilika mwaka 2006, ilikuwa ndiyo utafiti wa kwanza na wa kina wa dunia juu ya aina zote za ukatili dhidi ya watoto. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchunguza, kutoa taarifa na mapendekezo juu ya ukatili dhidi ya watoto unaofanyika katika hali mbalimbali ambazo watoto wanaishi —ikiwa ni pamoja na majumbani na kwenye familia, mashuleni, mfumo wa malezi na wa kutoa haki, sehemu za kazi na katika jamii.