MCDGC Publication

PRESS CONFERENCE - SIKU YA MTOTO WA AFRIKA 2016

Tarehe 16 Juni, 2016 ni kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Siku hii huadhimishwa na nchi zote wanachama wa Umoja wa Afrika kwa mujibu wa Azimio lililopitishwa na nchi 51 za Umoja huo mnamo mwaka 1990. Azimio hili lilipitishwa kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya watoto wa shule yaliyofanywa na utawala wa Makaburu katika kitongoji cha Soweto, Afrika ya Kusini tarehe 16 Juni 1976. Katika tukio hilo la kusikitisha, inakadiriwa kuwa watoto wapatao 2,000 waliuwawa kikatili na utawala huo. Watoto hawa walikuwa kwenye harakati za kudai haki yao ya msingi ya kutobaguliwa kutokana na rangi yao.

Kusoma zaidi    Bofya Hapa