MCDGC Publication

Sera ya Taifa ya Wazee

Suala la uzee na kuzeeka limekuwa lenye umuhimu mkubwa kwa jumuiya ya kimataifa hasa kuhusiana na mitazamo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Taarifa za umoja wa mataifa (1999) zinaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la idadi ya wazee Duniani. Ongezeko hili linaonekana zaidi katika nchi zinazoendelea ambapo viwango vya ongezeko havilingani na uwezo wa rasilimali zilizopo kuwahudumia katika nyanja za afya, lishe na huduma nyingine za msingi kwa maisha ya binadamu.

Kulingana na taarifa hizo, mwaka 1950, Umoja wa Mataifa ulikadiria kuwepo kwa watu millioni 200 wenye umri wa miaka 60 na zaidi. Mwaka 1975, idadi hiyo iliongezeka na kufikia millioni 350. Idadi hiyo inategemewa kuongezeka na kufikia milioni 625 ifikapo mwaka 2005.