MCDGC Publication

TAARIFA KWA UMMA (USAJILI WA NGOs)

Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali itaendesha zoezi la usajili wa Mashirika yaliyosajiliwa awali chini ya Sheria nyingine kama vile “Societies Act Cap 337” (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch); “Trustees’ Incorporation Act Cap. 318 (RITA); na The Companies Act Cap 212 (Msajili wa Makampuni-BRELA) ambazo zinatakiwa kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019. Bofya hapa kusoma zaidi