MCDGC Publication

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Wizara ya maendeleo ya jamii,na Watoto inakaribisha maombi ya nafasi ya kazi zilizo orodheshwa hapo chini kutoka kwa Watanzania kwa kuzingatia mashartimuhimu yafuatayo:-

(i). Maombi yaambatanishwe na nakala za Vyeti vya kuhitimu mafunzo na vya kidato cha IV na
VI, pamoja na nakala mbili za picha za mwombaji kipimo cha “Passport”,
(ii). Wawe wenye umri wa kuzaliwa usiozidi miaka 45 kwa wasio watumishi wa umma.
(iii). Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 11 Desemba, 2009.

1. AFISA UTUMISHI DARAJA II TGS.D (NAFASI 2)
(a). Sifa: Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya sayansi ya jamii au sanaa kutoka katika
Vyuo.
Vikuu vinavyotambuliwa na serikali ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya
Zifuatazo :
- Menejmenti ya Rasilimali watu (Human Resources Management)
- Elimu ya jamii (Sociology)
- Utawala na uongozi (Public Administration)
- Mipango ya utumishi(Manpower Planning)
Wawe na ujuzi wa kompyuta.

2. MSAIDIZI WA OFISI (TGOS.A)NAFASI 13.
Sifa:Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri katika masomo ya kingereza,
Kiswahili na Hisabati.

(c) KITUO CHA KAZI – VYUONI NA FDC.
Mabughai,Malampaka,Mbiga ,Nandembo, Kiwanda, Msaginya , Mwanya, Handeni, Rubondo, Nzega, Mlale, Msingi, Sikonge, Muhukuru, Newala na Masasi.

3. DEREVA DARAJA LA II (TGOS A) (NAFASI 6)
Sifa: Kuhajiriwa wenye cheti cha mtihani wa kudato cha IV wenye leseni daraja “C” ya undeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usio pungua miaka mitatu bila kusababisha ajali wenye cheti cha majaribio ya ufundi daraja la II

(c). KITUO CHA KAZI MAKAO MAKUU YA WIZARA NA CHUO CHA MWANHALA

4. MHUDUMU WA JIKONI / MESS DARAJA II (TGOS. A) NAFASI 50
Sifa: Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne wenye uzoefu wa kazi muda usio pungua miaka mitatu.

KITUO CHA KAZI - VYOUNI - CDTI NA FDC
Sikonge, Chilala, Sofi, Bariadi, Same, Sengerema, Kilwa Masoka, Njombe, Kihinga, Ngara, Nandembo, Chisalu, Nzovwe, Karumo, Newala, Munguri, Katumbi, Mlale, Kasulu, Msinga, Kibondo, Nzega, Rubondo, Mwanva, Msaginya, Kiwanda, Mbinga, Mabughai, Urambo.

MLINZI DARAJA LA II - TGOS. A- (NAFASI26)
Sifa: Kuhajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliofuzu masomo ya ulinzi wa Mgambo JKT, Polisi au zima moto inayo tambuliwa na Serikali.

KITUO CHA KAZI – VYUONI – CDTI NA FDC
Mwanhala, Nzega, Mabughai, Mbinga,Nandembo, Msaginya, Handeni, Msingi, Kasulu, Katumba, Sikonge, Muhukuru, Karumo, Urambo, Nzovwe, Uyole, Tango, Mtawanya, Ngara, Kisangwa, Munguri, na Bariadi.
MCHAMBUZI MFUMO WA COMPYUTA II (Computer Systems Analyst II) DARAJA LA II - TGS.D (NAFASI I)
Sifa: Awe na shahada / Stashahada ya juu katika masomo ya Sayansi ya Computer kutoka kwenye tasisi/ chuo kinacho tambuliwa na Serikali.

AFISA MAENDELEO YA JAMII DARAJA LA II - TGS. D (NAFASI 30)
Sifa:Kuajiriwa mwenye Shahada / Stashahada ya juu ya Maendeleo ya jamii kutoka vyou vinavyo tambulika na Serikali kayika fani zifuatazo:-

KITUO CHA KAZI
Ngara,Sikonge, Sofi, Muhukuru, Mbinga, Nandembo, Masasi, Chala, Mtawanya, Kilwa Masoka, Ilula, Njombe, Nzovwe, Msaginya, Chala, Urambo, Mwanhala, Nzega, Msingi, Singida, Mwanva, Kiwanda, Bariadi, Mlampaka, Malya, Tarime, Musoma, Kisangwa, Rubonda, Karumo,Kihinga,Kasuli na Kibondo.

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU - DARAJA LA II- TGS.B (NAFASI 12)
Sifa: Walio hitimu kidato cha IV / VI wenye cheti cha utunzaji kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya, Masjala, Mahakama na Ardhi.

AFISA UGAVI MSAIDIZI - TGS B- (NAFASI 14)
Sifa: Wenye cheti cha National Store Keeping Certificate, au Foundation Certificate” kitolewacho na boma ya Taifa ya usimamizi wa vifaa au wenye cheti kinacho tambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa vifaa.
Wenye Diploma la kawaida ‘’Ordinary Diploma in Materials Management” kutoka chuo kinacho tambuliwa na Bodi ya Taifa ya usimamizi wa vifaa.

MSIMAMIZI WA MAKTABA (TGS. B) - (NAFASI 6)
Wawe na cheti cha mtihani wa Taifa kidato cha IV na kufaulu mafunzo ya wasaidizi wa Maktaba (National Library Assistants Certificate) yanayotolewa na Bodi ya Huduma ya Maktaba Tanzania au wenye cheti kinacho lingana na hicho.

MPISHIDARAJA LA II TGS.C (NAFASI 13)
Sifa: Wenye kuhitimu kidato cha IV walio faulu mafunzo ya cheti yasio pungua mwaka mmoja katika fani ya “Food Production”yatolewayo.

KATIBU MUHTASI DARAJA LA III (TGS. B) - NAFASI 10
Sifa: Wawe na Cheti cha kuhitimu mtihani wa Taifa wa kidato cha nne (IV), Kuhudhuria mafunzo ya Uhadhiri na kufaulu mitihani ya hatua ya tatu. Wawe wamefaulu Hatimkato ya Kiswahili Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo Kompyuta kutoka chuo chochote kinacho tambuliwa na Serikali kupata cheti katika program za ‘’Windows, Microsoft Office, Internet, E-Mail” na “Pablissher”

MCHUMI DARAJA II - TGS. D - (NAFASI YA 3)
Sifa: Wawe na shahada ya kwanza, ambao wamejiimarisha (Major) katika mojawapo ya fani zifuzo:-
(i) Uchumi (Economics)
(ii) Takwimu (Statistics)
(iii) Sayansi ya Uchumi, Kilimo (BSc. Agriculture Economics & Agribusneness) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Chuo kikuu cha Sokoine au Chuo kingine chochote kinacho tambulika na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

AFISA HABARI DARAJA LA II TGS. D – (NAFASI 2)
Sifa: Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu ua Uandishi wa Habari au sifa inayolingana nayo kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambulika na Serikali.

Maoni tote yatumwe kwa:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA NA WATOTO, S.L.P3448,
DAR ES SALAAM.