MCDGC Publication

WATENDAJI WA WIZARA WAKABIDHIANA VYUO VYA MAENDELEO YA WANANCHI

Erasto T. Ching’oro Msemaji Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto
Katika kutekeleza hati idhini (instrument) ya Serikali ya Awamu ya Tano, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga ameitikia muundo huo, kwa kukabidhi Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bibi Maimuna Tarish, leo jijini Dar es salaam.
Akipokea Vyuo hivyo, Katibu Mkuu Maimuna Tarish ameeleza kuwa uamuzi wa kuhamishia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kwenda Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia unalenga kuboresha utendaji uliokuwepo maana tayarai Vyuo hivi vilikuwa na ushirikiano na VETA katika utoaji wa mafunzo ya maaendeleo ya wananchi samambamba na mafunzo ya umahiri yanayosimamiwa na Wizara ya Elimu.
Akipokea Vyuo hivyo, Tarish ameeleza kuwa Wizara ya Elimu imejipanga kutumia Vyuo vya Mmaendeleo ya Jmaii kwa manufaa makubwa kwa kuendeleza malengo ya awali na kuhuisha mafunzo ili kukidhi mahitaji ya soko.
Ameongeza kuwa, ingawa Vyuo vimehamia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wataendelea kuwa na ushirikiano na Wizara ya Maendeleo ya Jamaii, Jinsia, Wazee na Watoto kwani anatambua kuwa watendaji wanao uzoefu uliotukuka katika kuhakikisha kuwa Vyuo hivi vinapanua fursa kwa Washiriki wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi za kuendelea na masomo ya ufundi katika ngazi mbalimbali.
Wakati wa Kupokea Vyuo hivyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga, amaeleza kuwa Mafunzo ya Elimu ya Wananchi yalianza kutolewa katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi tangu mwaka 1975 wakati huo vikiwa vyuo 25. Madhumuni ya mafunzo hayo yalikuwa ni kuwapatia wananchi stadi na maarifa ili waweze kujiajiri na kuajiriwa hivyo kuongeza kipato cha kaya na kupunguza umaskini.
Vyuo vya Maeendeleo ya Wananchi viliongezeka kutoka 25 hadi kufikia 55 ambavyo vimekabidhiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia tarehe 4 Novemba, 2106. Vyuo hivi kwa sasa vyote vinatoa mafunzo ya maarifa na ufundi stadi chini ya usimamizi wa VETA. Kozi nyingine mamalum pia zimeaanzishwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa mabinti waliokosa fursa ya elimu kutokana na mimba za utotoni. Elimu hii inatolewa kwa watoto wa kike ili waweze kuwa na uwezo wa kutimiza ndto zao na pia kujitegemea.
Kuhama kwa Vyuo hivi, ni fursa ya kupata rasilimali ya kuboresha miundo mbinu na mazingira ya ufundishaji katika vyuo hivyo ifikapo mwaka 2020, ili kutoa elimu yenye staha kwa vijana wetu. Uhamisho wa vyuo utawezesha Serikali ya Awamu ya Tano, kushughulikia changamoto zilizobainishwa ikiwa ni pamoja na upungufu watumishi na kuboresha mazingira ya vyuo ili kuongeza udahili. Vyuo hivi vinaumuhimu mkubwa kuwa na nguvu kazi ya ndani wakati Taifa linajiandaa kuwa na uchumi wa kati.
Ameongeza kuwa, anaamini kwa Wizara ya Elimu itaweka utaratibu murua wa kufikia vyuo vyote 55 nchini, vyenye jumla ya watumishi 826. Vyuo hivi vimekuwa na mafanikio makubwa ambapo wanafunzi wanaohitimu wanajiajiri na wengine kuingia kwenye ajira rasmi. Vyuo hivi vinatoa mchango mkubwa katika stadi za uongozi kwa wananchi na kuwa kitivo cha maendeleo, maarifa na huduma za kijamii katika Halmashauri husika.
Baada ya tukio hili, makabidhiano mengine yatafanyika kwa kuhusisha Mawaziri wenye dhamana ili kukamilisha uhamamisho huo, wakati shughuli nyingine za kiutendaji zikiendelea. Tukio hili limefanyika leo asubuhi katika ukumbi wa Wizara ya Elimu na kuhudhuriwa na watendaji wakuu wa Wizara zote mbili pamoja na Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu (Pwani) na Kisarawe kilichoko Dar es salaam.